Ingia

Karibu Tena, Rafiki. Ingia kuanza kusoma vitabu

JISAJILI

Ukimaliza kujisajili hapa, lipia riwaya kwa M-pesa!

Kurudisha Neno la siri

Fortgot your password? Don't worry we can deal with it

UTANGULIZI - MSAKO II - The Game

"JACOB, tumepata taarifa muhimu, zimethibitishwa na shirika la kijasusi la Urusi FSB ambalo zamani lilijulikana kama KGB kuwa, Rais Obama alipoingia madarakani, kwenye ile siku ambayo wenyewe huiita 'Baptism Day' ambayo ni siku ya 50 kila Rais mpya hukutana na vitengo vikuu viwili vinavyo shughulika na usalama wa Marekani kutokea nje ; Ujasusi (CIA) na kile cha operesheni maalum (Navy Seals), alikabidhiwa mafaili 15 yaliyokuwa na alama nyekundu. Kikao hicho kilifanyika PENTAGON kama kawaida ya utaratibu wao. Hadi ndugu Obama anamaliza muda wake, yasemekana mafaili matano pekee ndiyo yamemshinda kuyafunga. Kwa kifupi ndiye Rais aliyefanikiwa kufunga mafaili mengi zaidi katika historia ya nchi hiyo, akiwa amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na George Bush mkubwa. Mafaili yaliyobaki wazi ambayo ameshindwa kuyafunga ni Korea, Tanzania, Iran, Guantanamo Bay na DRC Congo.” Alieleza Bi. Anita wakati akipekuapekua nyaraka zilizokuwa mezani kwake. Mara kadhaa jicho lake lilielekea hadi kwenye kompyuta kubwa ambayo kioo chake kilikuwa ukutani. Alifungua baadhi ya nyaraka alizohifadhi na kuyaonesha majina ya mafaili kwa mpangilio.

“Jacob, sababu za kushindwa kufunga mafaili matatu zinajulikana, lakini kushindwa kufunga mafaili mawili yaani Tanzania na Congo DRC hazijawekwa wazi japo kuna dondoo moja tu imepatikana mpaka sasa. Kwa njia zetu uzijuazo, taarifa imevuja mahali ikiwa imeandikwa kuwa DRC Congo halijafungwa kwa sababu ya ubishi wa Kagame.” Alizidi kufafanua Bi. Anita. Wakati huo Jacob alivuta taswira na kuunganisha nukta za alichokuwa akiambiwa, bado hakupata msingi hasa wa nini kilikusudiwa katika wito huo..

“Jacob, kilichotushitua zaidi ni uwepo wa faili la Tanzania. Baada ya kujua kuna faili kama hilo ambalo kwa vyovyote litatua mezani kwa Rais mpya, kiu yetu kama taifa ni kujua ambacho kimo ndani ya faili hilo ili tuweze kuona nini cha kufanya ikilazimu ingali mapema. Serikali imeamua kuwa kitengo chetu kishirikiane na FSB ili kuweza kujua undani wa faili hilo kwa njia na gharama yoyote.” Bi. Anita aliendelea kueleza.

“Naam, endelea nakusikiliza mama.” Jacob alimtaka Bi.Anita kuendelea kumfahamisha ili apate kujua maudhui ya wito uliokatisha safari yake.

“Unaweza kufahamu kwa nini Urusi inaingia kwenye jambo hili kupitia kwa mashirika yake ya kijasusi na operesheni ?” Alihoji Bi. Anita yangali macho yake yakimtazama Jacob ambaye alikuwa ametulia akisikiliza kwa makini.

“Hata sielewi, pengine niweke wazi nitafahamu.” Alijibu Jacob kwa kifupi.

“Hapa jibu ni jepesi sana, mafahali wawili katika vita ya uchumi na kijeshi hawakai chungu kimoja. Hivyo adui wa Urusi hubadilika kuwa rafiki wa Marekani na kinyume chake kwa Marekani pia. Tunataka kujua ni nini kiko kwenye faili. Tukijua hilo tutajua tutegemee matendo gani toka kwa Marekani." Alisema Bi Anita, mkuu wa Ofisi Fukuzi, kitengo cha kijasusi cha nchi ambacho kiko maalumu kushughulika na mambo ambayo hayahitaji papara, yanahitaji mtu ambaye ni zaidi ya askari na mwanajeshi kuweza kuyashughulikia.

"Kidogo naanza kupata picha juu ya hili jambo. Unadhani kwa nini Urusi wamewasiliana nasi haraka namna hii? Maana sidhani kama wanahitaji msaada wetu, wanaweza kufanya vema zaidi mara mia kuliko sisi, sasa bado sitaki kuamini kuwa Urusi kaja kutupa taarifa bure. Nahisi kuna kitu wanahitaji kunufaika nasi!” Mpelelezi Jacob Matata alihoji akionyesha wasiwasi wake.
Badala ya kujibu swali, Bi. Anita alitoa picha moja ambayo aliiweka juu ya meza. Ilikuwa picha ya kijana mmoja mweusi. Picha ilikuwa yenye rangi nyeupe na nyeusi, lakini ilikuwa imechakaa sana. Pamoja na uchakavu wa picha yenyewe, ilitosha kumwambia Jacob Matata kuwa picha hiyo ilipigwa miaka mingi iliyopita.

"Nilipokupa maelezo ya awali nilidhani swali lako lingekuwa 'nitafikiaje faili lililoko Pentagon? Lakini umeuliza kwa weledi zaidi. Sasa kama ulidhani ndani ya faili hilo kuna maelezo yoyote hapo umekosea sana. Kitu pekee kilichomo ndani ya faili hilo ni hii picha wala si kingine. Katika kutafakari sana tumejiridhisha kuwa huyu mtu yuko hai kwa vile picha yake bado haijawekewa alama ya msalaba au X. Pia tumejiridhisha kuwa mtu huyu kwa jina anaitwa Samwel Mahona ambaye kwa sasa inadhaniwa kuwa ana kati ya miaka 75 hadi 85. Yuko wapi na anafanya nini hilo hatujui. Imefanyika juhudi ya kujua aliko na kile anafanya, lakini haijajulikana bado. Tujuacho ni kuwa, mtu huyu alizaliwa katika hospitali ya misheni pale Urambo, Tabora. Picha ya mtoto mmoja hapo ndiyo imeoana na picha hii. Ila faili lake halionekani ndani ya hospitali." Alieleza Bi. Anita. Kabla hajaendelea alikatishwa na Jacob aliyeuliza swali.

"Kama faili halionekani, mmelinganisha vipi hii picha ili kujua kuwa huyu ni Samwel Mahona. Je, mmefahamje kuwa alizaliwa Urambo, Tabora?”

"Kuna daktari mmoja wa kizungu aliyekuwa akiitwa Derek Hilton alikuwa na tabia ya kubandika picha za watoto wote waliozaliwa hospitalini hapo kwenye kuta za chumba kimoja cha nyumba aliyokuwa akiishi, hapo ndipo tumepata picha inayooana na hili jina." Bi. Anita alieleza.

"Naona kama kuna maandishi yaliyofifia kwenye picha hii. Hayasomeki haya!!” Jacob alisema huku akiikodelea macho ile picha na kuisogeza jirani zaidi na uso wake.

"Ndiyo, tumejaribu sana kuyasoma maandishi hayo hafifu kwa kutumia wataalamu wetu, ni kama yamendikwa neno Old Railway H. Lakini hiyo bado haijatusaidia lolote. Sasa nataka kwa kutumia maelezo haya, anza upelelezi ili tujue ndani ya faili kuna nini ambacho wao wanajua sisi hatujui. Sielewi hii ina uzito gani hadi iwe kwenye Mafaili ya kukabidhiwa 'Baptism Day’.” Bi. Anita alisema huku akimwangalia Jacob Matata kwa makini.


Ili uweze kuendelea kusoma Tuma Tsh. 5000 kwenda namba +255 762 204 166 ili uweze kusoma kitabu MSAKO II - The Game


RIWAYA ZA KUSISIMUA NA MAFUNZO

SAA 72 ZA KUFA NA KUPONA
SAA 72 ZA KUFA NA KUPONA
SAA 72 ZA KUFA NA KUPONA

Kurejea kwa yule mbabe wa kivita bwana Joseph Katanga huko Congo DRC kunasababisha hali ya wasiwasi mkubwa. ICC wanamwachia wakati ambapo kiongozi wa nchi hiyo anatarajiwa kutangaz

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
PATASHIKA
PATASHIKA
PATASHIKA

Furaha Kijana Maganga, ambaye amebakiza mwezi mmoja kuhitimu mafunzo yake ya Upadri anajikuta yuko katikati ya wimbi zito la maisha pale mtandao wa kijasusi na wahalifu wa kimatai

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
HEKA HEKA
HEKA HEKA
HEKA HEKA

Utangulizi

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
MKONO WA SHETANI
MKONO WA SHETANI
MKONO WA SHETANI

Furaha aliyokuwa nayo mkurugenzi wa shirika la JEPA, Bwana Makia Kimisa kutokana na kupokea hati za msaada wa kipesa wa mamilioni ya dola toka nchi wahisani inatoweka ghafula. Hii

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
MSAKO
MSAKO
MSAKO

Kugundulika kwa gesi katika pwani ya mji wa Mtwara nchini Tanzania kunakuja kama tumaini jipya la kiuchumi kwa serikali na raia wa kawaida. Kila upande unajawa matumaini ya kuishi

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
MSAKO II - The Game
MSAKO II - The Game
MSAKO II - The Game

"JACOB, tumepata taarifa muhimu, zimethibitishwa na shirika la kijasusi la Urusi FSB ambalo zamani lilijulikana kama KGB kuwa, Rais Obama alipoingia madarakani, kwenye ile siku amb

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
NI ZAMU YAKO KUFA
NI ZAMU YAKO KUFA
NI ZAMU YAKO KUFA

Katika kisa hiki safari ya mpelelezi Jacob Matata inaanzia pale anapoitwa na bosi wake na kutumwa Arusha kupeleleza tetesi za kuwepo kwa silaha za hatari katika jiji hilo. Jacob Ma

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000
PATAPOTEA
PATAPOTEA
PATAPOTEA

Taarifa ziliponifikia kwanza nilizipuuzia. Niliendelea na shughuli zangu kwani niliziona kuwa ni taarifa za ajabu na zisizo na msingi wowote. Lak

Endelea Kusoma

  • Tsh BURE
MDHAMINI
MDHAMINI
MDHAMINI

Watoto watano wa kiume walifunzwa na kulelewa mfumo wa kuruka na kuwinda kama wana wa Tai. Hii ikawafanya kuondokea kuwa mafundi sana katika masuala ya kupigana na kutumia silaha.

Endelea Kusoma

  • Tsh 5000